Urusi yaifungia DW kulipiza kisasi dhidi ya Ujerumani
3 Februari 2022Matangazo
Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema katika taarifa kwamba imeifunga ofisi ya Deutsche Welle nchini Urusi, na kuwanyanganya vibali wafanyakazi wake wote, na pia kuisimamisha matangazo ya kituo hicho kwenye ardhi ya Urusi.
Shirika la usimamizi wa vyombo vya habari la Ujerumani MARBB, na Kamisheni ya Leseni na usimamizi wa taasi za habari ZAK, zilisema kwamba shirika la Russia Today tawi la Ujerumani, haliwezi kurusha matangazo yake nchini Ujerumani kwa kutumia leseni ya Serbia.
Mkurugenzi Mkuu wa Deutsche Welle Peter Limbourg ameikosoa hatua ya Urusi ya kufungia ofisi ya DW mjini Moscow na kuitaja kama ya kupitiliza huku akiongeza kuwa DW itachukua hatua za kisheria dhidi ya hatua hiyo.
Chanzo: dpa