Urusi yafungia baadhi ya vyombo vya habari vya Ulaya
26 Juni 2024Matangazo
Hatua hiyo ni sehemu ya kulipiza kisasi kwa hatua iliyochukuliwa na Umoja wa Ulaya kuvipiga marufuku vyombo vya habari vya Urusi.
Maafisa wa Urusi wanasema idadi kubwa ya vyombo vya habari vya magharibi vinaeneza ripoti zisizo za kweli kuhusu kile Urusi inachosema ni oparesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine.
ICC yatoa waranti ya kukamatwa viongozi waandamizi wa Urusi
Marufuku hayo yanatokea baada ya Umoja wa Ulaya mnamo mwezi Mei kutangaza kuwa inaifunga kile walichokitaja kuwa mitandao minne ya propaganda inayohusishwa na Kremlin.
Umoja wa Ulaya ulieleza kuwa marufuku hiyo ililenga Sauti ya Ulaya, shirika la habari la RIA, na magazeti ya Izvestia na Rossiyskaya Gazeta.