1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi yafanya mazoezi ya kijeshi katika Bahari Nyeusi

Hawa Bihoga
21 Julai 2023

Jeshi la wanamaji la Urusi limefanya mazoezi makubwa ya kijeshi katika Bahari nyeusi, ikiwa ni siku chache baada ya taifa hilo kutangaza, litashughulika na meli zinazosafiri kuelekea Ukraine kwa njia ya bahari hiyo.

https://p.dw.com/p/4UDg3
Golf von Oman | Russland, China und Iran halten gemeinsame Marineübung ab
Picha: Northern Fleet Press Service/TASS/dpa/picture alliance

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema mazoezi hayo ya jeshi la wanamaji ni hatua ya kuziba baadhi ya njia katika Bahari Nyeusi ambayo inatumika kusafirisha nafaka kutoka Ukraine.

Zoezi hilo limekuja baada ya Moscow kutangaza maeneo makubwa ya Bahari Nyeusi kuwa ni hatari kwa urambazaji kufuatia kujiondoa katika mpango huo wa nafaka.

Soma pia:Urusi na China zafanya luteka za pamoja za kijeshi

Katika taarifa yake wizara hiyo imethibitishwa kwamba, boti ya Moscow ilifyatua moja kwa moja makombora ya kuzuia meli katika meli iliolengwa huko kaskazini magharibi mwa Bahari Nyeusi, na meli hiyo iliharibiwa vibaya kutokana na shambulio la kombora.

Mmoja wa wahudumu katika kikosi hicho cha wanamaji cha Moscow amesema, katika mazoezi ya leo, mashua mbili zilifanya shambulio la meliya adui wa kubuni.

 "Mazoezi ya mapigano yalifanyika kwa kutumia silaha za kombora."

Alisema wakati mazoezi ya kijeshi yakiendelea na kuongeza kwamba katika ufyatuaji wa makombora ulifanikiwa, adui wa kubuni aliangamizwa.

Soma pia:Urusi yazitahadharisha meli zinazotumia njia ya Bahari Nyeusi

Baada ya kujiondoa katika makubaliano ya kuwezesha usafirishaji salama wa nafaka kutoka Ukraine, Kremlin ilisema Jumatano kwamba, itazizingatia meli za mizigo zinazopelekwa Ukrainekupitia Bahari Nyeusi.

Kadhalika katika taarifa yake ilipiga marufuku shughuli za usafirishaji katika maeneo ya kaskazini magharibi na kusini mashariki mwa bahari.

Ukraine yasisitiza kuendelea kwa usafirishaji nafaka

Ukraine pia  ilipiga marufuku urambazaji kwenye sehemu ya kaskazini-mashariki ya Bahari Nyeusi na Mlango-Bahari wa Kerch karibu na Crimea, na kufanya urambazaji katika sehemu kubwa ya Bahari Nyeusi kuwa hatari kwa meli.

Ukraine  imeendelea kusisitiza kwamba itakuwa tayari kuendelea na mauzo ya nafaka kutoka bandari zake za kusini kufuatia Moscow kujiondoa katika makubaliano hayo.

Imetoa wito pia kwa Umoja wa Mataifa na nchi jiranikuwekwa kwa njia salama kwa mizigo kupitia doria za pamoja.

Zelenskiy amfuta kazi Balozi wake wa Uingereza

Rais Volodymyr Zelenskiy wa Ukraine amemfuta kazi Vadym Prystaiko kama balozi wa Ukraine nchini Uingereza leo Ijumaa, ikiwa ni siku chache baada ya mwakilishi huyo kumkosoa rais hadharani.

Themenpaket | Getreidehandel Getreide-Deal Grain deal Ukraine Russland
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Pool Philip Reynaers/belga/dpa/picture alliance

Amri ya rais, ambayo ilisema Prystaiko pia ameondolewa kama mwakilishi wa Ukraine katika Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Baharini, haikutoa sababu ya kufutwa kazi.

Soma pia:Zelensky amfuta kazi balozi wake nchini Uingereza

Katika mahojiano na shirika la habari la  Sky wiki iliyopita, Prystaiko aliulizwa kuhusu matamshi ya Waziri wa Ulinzi wa Uingereza anayemaliza muda wake Ben Wallace.

Mwanadiplomasia huyo, alipendekeza Kyiv ionyeshe shukrani zaidi kwa uwasilishaji wa silaha kutoka kwa washirika wake ili kupambana na vikosi vinavyoikalia kwa mabavu vya Urusi.

Agizo la Zelensky halikusema wazi ni naniangelichukua nafasi ya mwanadiplomasia huyo mzoefu na makamu waziri mkuu wa zamani ambaye, alishikilia wadhifa huo kama balozi nchini Uingereza kwa miaka mitatu.