1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi yaishambulia Ukraine kwa ndege zisizokuwa na rubani

2 Julai 2023

Jeshi la Ukraine limesema Urusi imefanya mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani nchini humo baada ya mapumziko ya siku 12, huku mifumo ya ulinzi wa anga ikifanikiwa kuharibu mashambulizi yote yaliyoelekezwa Kyiv.

https://p.dw.com/p/4TJpI
Ukraine Krieg l  Bergungsarbeiten nach  Raketenangriff in Kramatorsk
Picha: Narciso Contreras/AA/picture alliance

Katika ujumbe kupitia mtandao wa telegram, mkuu wa utawala wa jeshi la Kyiv kanali jenerali Serhiy Popko, aliandika kuwa kuna shambulio lingine kutoka kwa adui dhidi ya Kyiv na kuongeza kuwa kwa sasa, hakuna taarifa kuhusu kuwepo kwa majeruhi au uharibifu.

Mashuhuda walisikia milipuko

Mashuhuda waliozungumza na shirika la habari la Reuters, wanasema walisikia milipuko inayofanana na sauti za mifumo ya ulinzi wa anga ikilenga mashambulizi yaliyoelekezwa kwenye mji huo. Eneo la Kyiv na maeneo kadhaa ya Kati na Mashariki mwa Ukraine yalikuwa chini ya tahadhari za uvamizi wa anga kwa takriban saa moja baada ya saa nane alfajiri nchini humo.