1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Urusi yaendelea 'kuitwanga' Ukraine

27 Januari 2023

Jeshi la Ukraine limesema kuwa hatari ya mashambulizi ya anga ya Urusi imeendelea kuwa ya juu, wakati Urusi ikizidisha makombora yanayoangushwa na ndege zisizo rubani.

https://p.dw.com/p/4MmR7
Ukraine | Zerstörung in der Stadt Hlevakha
Picha: Valentyn Ogirenko/REUTERS

Mashambulizi hayo yameongezeka siku moja baada ya makombora na ndege zisizo na rubani za Urusi kuwaua watu wapatao 11 ikiwa ni katika kujibu hatua ya washirika wa Magharibi wa Ukraine kuahidi kuipatia nchi hiyo vifaru.

Urusi pia imefanya mashambulizi 37 ya anga, 17 kati yake yakiwa kwa kutumia ndege zisizo na rubani aina ya Shahed zilizotengenezwa Iran.

Soma zaidi: Ukraine yakataa ombi la Putin la kusitisha mapigano kwa muda
UN: Raia 18,000 wauawa au kujeruhiwa Ukraine

Urusi yafanya mashambulizi kutaka kuukamata mji wa Bakhmut

Jeshi la Ukraine limesema limedungua makombora 47 ya Urusi kati ya 59. 

Wakati huo huo, Shirika la Kimataifa la kudhibiti matumizi ya Nishati ya Nyuklia, IAEA, limesema mashambulizi yamesikika karibu na kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia.

Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban amesema leo kuwa nchi yake itapinga vikwazo vyovyote vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Urusi ambavyo vinaathiri nishati ya nyuklia.