Urusi yadaiwa kuteka maeneo ya Ukraine mwezi Julai
31 Julai 2024Uchambuzi huo, unaotokana na data kutoka Taasisi ya Utafiti wa Vita (ISW) yenye makao yake nchini Marekani, unaonyesha ongezeko ikilinganishwa na mwezi uliopita lakini ufanisi mdogo ikilinganishwa na mwezi Mei, wakati vikosi vya Urusi vilipoanzisha mashambulizi ya ardhini katika eneo la mpakani la Kharkiv, ambayo yamesitishwa kwasasa.
Maafisa: Urusi imefanya mashambulizi ya droni mjini Kyiv
Katika mwezi huo vikosi vya Urusi vilikamata kilomita za mraba 449, wastani wa kilomita za mraba 14.5 kwa siku, huu ukiwa ufanisi mkubwa wa mwezi tangu Machi 2022, mara tu baada ya Rais Vladimir Putin kuamuru uvamizi wa Ukraine.
Tangu mwanzoni mwa mwaka 2024, Urusi imekamata kilomita za mraba 1,246 za eneo la Ukraine, zaidi ya kilomita za mraba 584 zilizokamatwa katika mwaka mzima wa 2023.