Urusi yadai kutwaa mji muhimu magharibi ya Ukraine
4 Julai 2024Matangazo
Mji wa Chasiv Yar upo umbali wa kilomita 20 kuelekea magharibi mwa mji wa Bakhmut, ambao ulitwaliwa na vikosi vya Urusi mwaka uliopita.
Soma zaidi: Mashambulizi ya Urusi yasababisha vifo vya watu 3 Dnipro
Pande zote mbili zinauchukulia mji wa Chasiv Yar kama eneo la kimkakati ambalo linaweza kutumiwa na Urusi kama sehemu ya kuanzisha mashambulizi kuelekea upande wa magharibi mwa Ukraine kupitia mkoa wa Donetsk kuelekea miji ya Kramatorsk na Sloviansk.
Afisa habari wa Kikosi cha 24 cha Ukraine, Ivan Petrechak, amesema hali ni ngumu ingawa kikosi chake bado kipo kwenye eneo hilo.