1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yabadilishana wafungwa na nchi za Magharibi

1 Agosti 2024

Mwandishi wa habari wa gazeti la Wall Street Evan Gershkovich na mwanajeshi wa zamani, Paul Whelan wote raia wa Marekani, ni miongoni mwa wafungwa 26 walioachiliwa Alhamisi.

https://p.dw.com/p/4j0w1
Mpango wa kubadilishana wafungwa
Wafungwa 26 waachiliwa katika makubaliano ya kubadilishana wafungwa kati ya Urusi na nchi kadhaa za magharibiPicha: AP/picture alliance

Mwandishi wa habari wa gazeti la Wall Street Evan Gershkovich na mwanajeshi wa zamani, Paul Whelan wote raia wa Marekani, ni miongoni mwa wafungwa 26 walioachiliwa Alhamisi, katika makubaliano ya kubadilishana wafungwa kati ya Urusi na nchi kadhaa za magharibi, ofisi ya rais wa Uturuki imesema.

Gershkovich na ameachiliwa wiki chache baada ya mahakama ya Urusi kumuhukumu kifungo cha miaka 16 jela kwa kosa la ujasusi, sawasawa na mwanajeshi huyo, ingawa wao pamoja na Marekani wanakana.

Soma pia: Urusi yamhukumu kifungo cha miaka 16 mwandishi wa Marekani

Taarifa ya Uturuki imesema mabadilishano hayo yaliyofanywa na idara ya ujasusi ya Uturuki, MIT yalihusisha wafungwa kutoka Marekani, Ujerumani, Poland, Slovenia, Norway, Belarus na Urusi.