1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaadhimisha miaka 63 ya ushindi wake dhidi ya Manazi wa Kijerumani

9 Mei 2008

Rais Mpya wa Urusi Dmitry Medvedev na Waziri Mkuu wa Nchi hiyo Vladimir Putin, wamehudhuria gwaride kubwa la Kijeshi lililofanyika kwenye uwanja mwekundu mjini Moscow.

https://p.dw.com/p/DxGG
Rais wa Urusi, Dmitry Medvedev .Picha: AP

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Bunge la Urusi kumuthibitisha Putin kuwa ni Waziri Mkuu.

Washika bendera waliongoza gwaride hilo ikiwa ni ishara ya kumbukumbu ya miaka sitini na tatu ya Ushindi wa Urusi dhidi ya Vita vyake na Ujerumani wakati wa Vita Kuu ya pili.

Kiasi chaa wanajeshi elfu nane walitarajiwa kushiriki katika gwaride hilo. Rais Medvedev pamoja na Waziri Mkuu Putin, wamehudhuria gwaride hilo wakiwa pamoja na mamia ya maveterani wa Vita na wageni mbalimbali.

Makombora ya nyuklia na vifaru vilioneshwa kwenye gwaride la mjini Moscow kwa mara ya kwanza tokea kusambaratika himaya ya kisoviet lakini rais mpya wa Urusi Dimitri Medvedev ameyaonya mataifa mengine dhidi ya kuwania malengo yanayoweza kusababisha vita.

Vikosi vya wanajeshi alfu nane waliokuwa wanatembea mwendo ya kunyata kwenye uwanja mwekundu,vilifuatiwa na maonyesho ya silaha nzito ikiwa pamoja na makombora ya masafa marefu yaliyofunikwa na kivuli cha ndege za kivita zilizokuwa katika anga ya mji wa Moscow.

Akikagua gwaride hilo kwa mara ya kwanza kama amiri jeshi ,rais Medvedev wa Urusi ameonya dhidi ya matendo yanayoweza kusababisha vita duniani kote.

Katika kile kilichoonekana kama ,kupinga sera ya nje ya utawala wa rais Bush na hatua ya nchi za magharibi ya kutambua uhuru wa jimbo la Kosovo, kiongozi huyo mpya wa Urusi amezilaumu nchi zjnazojiingiza katika mambo ya ndani ya nchi zingine.

Gwaride hilo kubwa la kijeshi katika kuadhimisha mwaka wa 63 tokea majeshi ya kisoviet yatokomeze majeshi ya mafashisti wa kijerumani ,linaashiria ujasiri wa Urusi baada ya miaka minane chini ya uongozi wa Vladimir Putin, aliye endesha siasa zilizosababisha mikwaruzano na nchia za magharibi.

Gwaride hilo limefanyika muda mfupi baada ya Urusi kuwafukuza mabalozi wawili wa Marekani.

Hapo awali Marekani ilimfukuza nchini, jasusi mmoja wa kirusi.

Hata hivyo gharama za maandalizi ya waride hilo zinatajwa kuwa zilikuwa kubwa zaidi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mjini Moscow, gharama za kukarabati barabara za mitaa peke yake kwa ajili ya kupitisha vifaa vizito vya kijeshi zilifikia dola milioni sitini.