Urusi na China zapinga rasimu ya azimio la Marekani
23 Machi 2024China na Urusi pamoja na mataifa mengine ya Kiarabu yamesema lugha iliyotumika kwenye rasimu hiyo ni dhaifu mno na kamwe hailengi kuiwekea Israel shinikizo lolote.
Licha ya pingamizi la Urusi na China, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema wanadiplomasia wataendelea na juhudi za kutafuta mwafaka juu ya maandishi sahihi yanayokubalika na kila upande kwenye rasimu hiyo ya azimio.
Soma pia: Mashambulizi ya Israel katika hospitali ya al-Shifa yaua watu 140
Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Vasily Nebenzia amesema kwa jinsi maandishi yalivyo kwenye rasimu hiyo, itafungua mlango kwa Israel kuendelea kuvunja sheria bila ya kujali.
Mwanadiplomasia wa Marekani Antony Blinken amezishtumu China na Urusi kwa kutumia nguzu zao za kura ya turufu kwa maslahi yao binafsi huku kundi la Hamas likikaribisha uamuzi uliochukuliwa na Beijing na Moscow.