1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi: Maelfu wakusanyika kumzika Mikhail Gorbachev

Zainab Aziz Mhariri: Sylvia Mwehozi
3 Septemba 2022

Maalfu ya warusi leo wametoa heshima zao za mwisho kwa Mikhail Gorbachev aliyekuwa kiongozi wa mwisho wa Umoja wa Kisoviet aliyechukua hatua zilizomaliza vita baridi barani Ulaya.

https://p.dw.com/p/4GO8p
Moskau Trauerfeier für Michail Gorbatschow | Dmitri Medwedew
Picha: Ekaterina Shtukina/Sputnik/REUTERS

Hata hivyo mazishi yake hayakuwa ya kiserikali. Gorbachev amezikwa mahala ambapo viongozi wa hapo awali wa Umoja wa Kisoviet wamezikwa ikiwa pamoja na Lenin, Stalin na Brezhnev.

Rais wa Urusi Vladmir Putin hakuhudhuria mazishi ya Gorbachev na amesema kusambaratika kwa Umoja wa Kisoviet ni maafa makubwa ya siasa za kikanda. Hata hivmnamo siku ya Alhamisi kwa faragha, rais Putin aliweka shada la maua kwenye jeneza la Gorbachev katika hospitali ambako alifariki. Makamu wa rais wa Urusi Dmitry Medvedev alihudhuria mazishi hayo.Viongozi wa nje waliohudhuria walikuwa pamoja na waziri mkuu wa Hungary Victor Orban na wawakilishi wa kibalozi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin akitoa heshima zake za mwisho kwa Mikhail Gorbachev.
Rais wa Urusi Vladimir Putin akitoa heshima zake za mwisho kwa Mikhail Gorbachev.Picha: Russian pool/AP/picture alliance

Baadhi ya watu wanamlaumu Gorbachev kwa kuanzisha mageuzi yaliyosababisha vurumai za kiuchumi na pia kusababisha kusambaratika kwa Umoja wa Kisoviet. Hata hivyo marehemu kiongozi huyo anaheshimiwa miongoni mwa nchi za magharibi kwa kwa kuanzisha sera zilizovimaliza vita baridi barani Ulaya. Wajerumani ndiyo walionufaika kwa kiwango kikubwa na sera za Gorbachev. Ujerumani iliyogawanywa  baada ya kumalizika vita vikuu vya pili iliweza kuungana tena.

Mikhail Gorbachev aliingia madarakani mnamo mwaka 1985 na kuanza kujenga ujasiri wa kuleta mageuzi. Hakuna kiongozi mwingine wa Umoja wa Kisoviet wa hapo awali aliyethubutu kupitia njia hiyo. Hata hivyo  hakuweza kuepusha kusambaratika kwa umoja huo.

Kushoto: Rais wa zamani wa Marekani marehemu Ronald Reagan. Kulia: Kiongozi wa zamani wa Umoja wa Kisovieti Mikhail Gorbachev.
Kushoto: Rais wa zamani wa Marekani marehemu Ronald Reagan. Kulia: Kiongozi wa zamani wa Umoja wa Kisovieti Mikhail Gorbachev.Picha: AP

Nchi zilizokuwamo katika umoja huo zilianza kujitangazia uhuru. Hadi kufika mwaka 1991 Umoja wa  Kisoviet ulikata roho. Hata hivyo nje ya Urusi Gorbachev aliheshimiwa kwa kiwango kikubwa.Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema Gorbachev aliubadilisha mkondo wa historia. Rais wa Marekani Joe Biden amemwita Gorbachev kuwa kiongozi adimu.

Kulia: Binti wa Mikhail Gorbachev, Irina Gorbacheva-Virganskaya kwenye maziko ya baba yake.
Kulia: Binti wa Mikhail Gorbachev, Irina Gorbacheva-Virganskaya kwenye maziko ya baba yake.Picha: Sergei Bobylev/Tass/dpa/picture alliance

Gorbachev alifariki Jumanne iliyopita baada ya kuugua  kwa muda mrefu.Alitimiza umri wa miaka 91. Hayati kiongozi huyo mashuhuri amezikwa karibu na kaburi la mkewe Raisa, kwenye maziara ya Novodevichy mjini Moscow.

Vyanzo:/AP/RTRE