1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi kumchunguza mwandishi wa DW na kituo cha 1+1

27 Agosti 2024

Urusi imesema leo Jumanne kwamba, imeanzisha uchunguzi dhidi ya waandishi habari wa Deutsche Welle na kituo cha 1+1 cha Ukraine,kwa kuingia katika maeneo la jimbo la Kursk la Urusi yanayodhibitiwa na Ukraine.

https://p.dw.com/p/4jybA
DW Bonn
Majengo ya DW BonnPicha: Florian Görner/DW

Urusi imesema leo Jumanne kwamba, imeanzisha uchunguzi dhidi ya waandishi habari wa Deutsche Welle na kituo cha 1+1 cha Ukraine,kwa kuingia katika maeneo la jimbo la Kursk la Urusi yanayodhibitiwa na Ukraine.

Katika taarifa yake,idara ya usalama ya Urusi FSB  imesema inawachunguza mwandishi wa habari wa Deutsche Welle, Nick Connoly na Natalia Nagornaya  wa kituo cha 1+1 wanaotuhumiwa kuingia katika ardhi ya Urusi kinyume cha sheria baada ya kuanza operesheni ya kijeshi ya Ukraine mwanzoni mwa mwezi huu.Urusi yawapokonya vibali waandishi habari wa DW Moscow

Waandishi habari wengine watano ambao sio raia wa Urusi tayari wanachunguzwa na huenda wakakabilia na kifungo cha miaka 5 jela ikiwa watakutwa na hatia.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW