1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Urusi inataka kutia shubiri mahusiano yake na Uturuki?

17 Agosti 2023

Mapema wiki hii wanajeshi wa Urusi walivamia na kuikagua meli karibu na pwani ya Uturuki hatua inayovisogeza vita vya Ukraine karibu na mpaka wa Uturuki ambayo inafanya juhudi kuirudisha urusi kwenye mkataba wa nafaka.

https://p.dw.com/p/4VHa2
Ukraine | Getreideabkommen | Frachtschiff Tq Samsun Odessa - Istanbul
Picha: Serhii Smolientsev/REUTERS

Wanajeshi wa Urusi kwa kutumia helikopta waliivamia meli hiyo yenye makao yake nchini Uturuki umbali wa kilometa 60 kutoka pwani ya Uturuki kwenye eneo la bahari la kimataifa, lakini karibu na Istanbul. Urusi imesema ilifanya ukaguzi huo kabla ya meli hiyo kuanza safari ya kuelekea Ukraine. 

Uturuki, ambayo inashika nafasi ya pili kwa ukubwa wa jeshi katika NATO, haijatoa kauli yoyote hadharani juu ya kadhia hiyo.

Hata hivyo wachambuzi wanasema mkasa huo ni mtihani kwa rais wa Uturuki Tayyip Erdogankatika azma ya rais huyo juu ya kudumisha uhusiano mzuri na rais wa Urusi Vladimir Putin ambaye amemwalika nchini Uturuki mwezi huu ili kujadiliana kuhusu kuanza tena kuutekeleza mkataba juu ya usafirishaji  wa nafaka uliofikiwa kutokana na usuluhishi wa Umoja wa Mataifa.

Mkataba huo ulihakikisha mauzo ya ngano kutoka Ukraine.

Soma pia:Putin asema Urusi iko tayari kurejea katika usafirishaji wa nafakai

Mchambuzi wa siasa za kikanda nchini Uturuki, Yoruk Isik amesema uchokozi wa aina uliofanywa na Urusi karibu na Uturuki unaonesha kwamba Urusi haiheshimu haki za Uturuki.

Kunyamaza kimya kwa Uturuki ni jambo la kushangazalakini bado inatumai kwamba rais Putin atafanya ziara nchini Uturuki  na kwamba Urusi itarejea kwenye mkataba juu ya usafirishaji  wa ngano ya Ukraine.

Tangu Urusi ijitoe kwenye makubaliano ya usafirishaji wa  nafaka mwezi uliopita, nchi hiyo na Ukraine zimetoa maonyo  na kila upande umeshambulia meli za upande mwingine na hivyo kusababisha wasiwasi juu ya usafirishaji baharini kuwa  wa hatari kwa biashara kwenye eneo lote la bahari nyeusi.

Uturuki haiafiki njia mbadala usafirishaji nafaka?

Wakati Ukraine na baadhi ya mataifa ya Magharibi yanapigia  debe njia mbadala kwa ajili ya kusafirisha bidhaa za Ukraine, Uturuki ambayo pia ina mahusiano mazuri na nchi hiyo, kimya kimya inapinga njia hizo  mbadala kutokana na sababu za kiusalama.

Usbekistan l Gipfeltreffen in Samarkand l  Erdogan und Putin
Rais wa uturuki Recep Tayyip Erdogan na rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Alexander Demianchuk/TASS/dpa/picture alliance

Uturuki inazitaka nchi za magharibi ziyazingatie baadhi ya matamshi ya Urusi. Uturuki pia inaitaka Urusi iweke kando baadhi ya matamshi yake ili makubaliano yafikiwe ya kuanza tena kusafirisha nafaka, chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa na Uturuki.

Mapema wiki hii Urusi ilishambulia sehemu muhimu za bandari  licha ya Ukraine kusema kwamba meli yake ya kontena  iliongòa nanga kutoka Odesa, yaani njia mojawapo mbadala.

Soma pia:Zelensky azungumza na Erdogan kuhusu kufufua mkataba wa kusafirisha nafaka

Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia biashara na maendeleo amesema asasi hiyo inawasiliana na  pande zote mbili katika juhudi ya kuzirudisha kwenye  mazungumzo, ingawa hatua hiyo ni ngumu hasa baada ya miundombinu ya nafaka kushambuliwa kwa mabomu.

Urusi na Ukraine wazalishaji wakubwa wa ngano duniani wanatumia bahari nyeusi na njia za Uturuki kusafirisha  nafaka kote duniani.

Hata hivyo kila upande umetishia kushambulia meli za mwenzake, baada ya mkataba wa nafaka kusambaratika baada ya mwaka mmoja tangu kufikiwa.

Hali hiyo imesababisha kupanda kwa bei za bidhaa duniani. Kila upande umesema utazingatia meli za upande mwingine kuwa za kivita.

Wachambuzi: Uturuki izungumze na mataifa ya Magharibi zaidi

Ni changamoto kubwa kwa Uturuki kujaribu kutoa sauti yake ili isikike juu ya suala la meli iliyovamiwa na kukaguliwa na wanajeshi wa Urusi mapema wiki hii.

Uturuki yenyewe inapeleka silaha kwa Ukraine licha ya kudai kwamba haiuungi  mkono upande wowote katika vita vya Ukraine.

Uturuki imechukua dhima ya kuwezesha mazungumzo kati ya  Urusi na Ukraine.Imepinga uvamizi wa Urusi, lakini pia imepinga vikwazo vilivyowekwa na nchi za magharibi na imeongeza ushirikiano wa kiuchumi na Urusi.

Imepinga uvamizi wa Urusi, lakini pia imepinga vikwazo vilivyowekwa na nchi za magharibi na imeongeza ushirikiano wa kiuchumi na Urusi.

Soma pia:Urusi yazitahadharisha meli zinazotumia njia ya Bahari Nyeusi

Urusi imesema itarejea katika mkataba wa nafaka ikiwa nchi za magharibi nazo zitatimiza wajibu wao, ikiwa pamoja na  kuiwezesha Urusi pia isafirishe nafaka na mbolea yake.

Pia Urusi inazitaka nchi za magharibi ziondoe vikwazo zilizoweka dhidi ya Urusi katika mfumo wa malipo wa SWIFT.

Wachambuzi wanasema rais Erdogan anapaswa kufanya juhudi kubwa zaidi katika kuzirai nchi za magharibi badala ya Urusi.

Meli ya UN iliyobeba nafaka yaelekea Afrika kutoka Ukraine