1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi iko tayari kufanya kazi na kiongozi yeyote wa Marekani

18 Julai 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema taifa lake lipo tayari kufanya kazi na kiongozi yeyote atakaechaguliwa na Wamarekani katika uchaguzi mkuu wa Novemba wa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4iRY3
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Lavrov atembelea Marekani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov (Kulia) na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran Ali Bagheri Kani wakipeana mikono wakati wa mkutano kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Julai 17.2024Picha: Valery Sharifulin/TASS/dpa/picture alliance

Amesema lakini kwa zingatio la aliye tayari kushiriki katika "mazungumzo ya usawa, yenye kuheshimiana kwa pande zote."

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, alisema katika kipindi cha utawala wa Rais Donald Trump kulikuwa na mazungumzo yanayoendelea licha ya vikwazo vingi vya Marekani dhidi ya taifa hilo.