1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urejeshaji wa mpakani wa EU: Sera "kivuli" ya uhamiaji?

Ella Joyner Iddi Ssessanga
8 Agosti 2023

Neno urejeshaji au "pushback" limeingia katika kamusi ya EU pamoja na mamia ya maelfu ya watu ambao wametafuta hifadhi katika kanda hiyo tangu 2015. Wanaharakati wanasema "pushback" sasa zimekuwa utaratibu na sera halisi

https://p.dw.com/p/4UvNr
Nordmazedonien | Frontex-Beamte treffen mazedonische Polizei
Picha: Innenministerium Nord-Mazedonien

'Urejeshaji' ni nini?

Neno "pushback," au "urejeshaji nyuma" ingawa linatumiwa sana na mashirika ya haki za binadamu sawa na maafisa wa serikali, ukweli ni kwamba halina ufafanuzi maalum wa kisheria. Katika ripoti ya mwaka wa 2021, mtaalamu wa Umoja wa Mataifa Felipe Gonzalez Morales alizielezea kama "hatua, vitendo au sera zinazopelekea kuondolewa kwa wahamiaji, mmoja mmoja au kwa makundi, bila tathmini ya kibinafsi kulingana na wajibu wa kuzingatia haki za binadamu na dhamana ya mchakato unaostahili."

Haya yanaweza kufanywa na watendaji wa serikali, kama vile polisi, walinzi wa mpaka au wanajeshi au watendaji wasio wa kiserikali, ambao wanaweza kujumuisha wanajeshi, wafanyakazi wa usalama wa binafsi au wafanyakazi kwenye usafiri wa kibiashara, Morales alibainisha.

Wakati urejeshaji haujafafanuliwa katika sheria ya kimataifa, huwa unakwednda kinyume na kanuni zilizoainishwa vyema na wajibu wa kisheria.

Mataifa ya Umoja wa Ulaya yana haki ya kulinda mipaka yao ya kitaifa na kuwakatalia kuingia watu binafsi wanaovuka mipaka kinyume cha sheria, lakini kama watia saini wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi wa 1951 na Mkataba wa Ulaya wa Haki za binadamu pia wanalazimika kuheshimu ahadi kadhaa.

Greece Is Expanding With Concrete Filled Fence And Police Patrols The Land Borders With Turkey
Maafisa wa polisi wa mpaka wa Ugiriki wakishika doria kando ya uzio wa chuma karibu na mto Evros kati ya Ugiriki na Uturuki ili kuzuia wahamiaji kuingia bila kibali.Picha: Nicolas Economou/NurPhoto/picture alliance

Hizi ni pamoja na, kulingana na Morales, marufuku ya ufukuzwaji jumla, haki ya kutafuta hifadhi na kanuni ya kutorudisha, ambayo inakataza kuwarudisha wanaotafuta hifadhi katika nchi ambayo itakuwa hatari kwao.

Urejeshaji unafananaje?

Urejeshaji nyuma unaweza kuchukua mifumo mbalimbali. Kwa wepesi zaidi, inaweza kuwa mlinzi mmoja wa mpakani anaemzuwia mtu mmoja anaenuwia kuomba hifadhi kuvuka kwa kutumia vurugu (au kutishia kutumia vurugu), iwe ya kimwili au kwa maneno. 

Mnamo mwezi Mei, gazeti la kila siku la Marekani la New York Times lilichapisha video za kushtua zinazodaiwa kuonyesha ufukuzwaji wa kinyume cha sheria wa kundi la watu wanaotafuta hifadhi, wakiwemo watoto, nchini Ugiriki.

Soma pia: Kufuatia mfufulizo wa kashfa za uhamiaji Waziri Mkuu wa Uholanzi atangaza kuachana na siasa

Watu hao walipakiwa kwanza kwenye gari lisilokuwa na alama, kisha wakawekwa kwenye boti ya walinzi wa pwani ya Ugiriki, wakashushwa kwenye boti la dharura na kuliachia baharini pasina wafanyakazi, kulingana na gazeti hilo. Hatimaye walichukuliwa na walinzi wa pwani wa Uturuki, ulihitimisha uchunguzi huo - uliochukuliwa kuwa ushahidi kamili zaidi wa vidio wa urejeshaji kufikia sasa.

Baadhi ya matukio ya hali ya juu zaidi yamehusisha makundi makubwa zaidi ya watu na hali ngumu zaidi. Mfano ni mfadhaiko mkubwa kwenye mpaka wa Uhispania na Morocco katika eneo la Uhispania la Melilla Juni mwaka jana. Uchunguzi wa kina wa shirika la habari la Uingereza BBC, miongoni mwa mambo mengine, uligundua kuwa sio tu kwamba watu 24 walikufa, zaidi ya watu 450 walikuwa wamerudishwa nyuma kutoka eneo la Uhispania hadi Morocco wakati wa machafuko.

Ni wapi madai ya urejeshaji unaodaiwa yamerikodiwa?

Muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali, Mtandao wa Kufuatilia Ghasia Mipakani, unadai kukusanya ushuhuda wa kufukuzwa kinyume cha sheria na kuathiri takriban watu 25,000 tangu 2017, gazeti la kila siku la Uingereza la The Guardian liliripoti mwishoni mwa mwaka jana.

Matukio ya kurejeshwa nyuma yameorodheshwa katika maeneo mbalimbali kwenye mipaka ya nje ya Umoja wa Ulaya katika muongo mmoja uliopita, kulingana na Stephanie Pope, mtaalam wa uhamiaji katika shirika lisilo la kiserikali la Oxfam.

Griechenland, Thessaloniki | Flüchtlinge auf der Balkan Route
Wanaume wanaotafuta hifadhi kama wanavyoonekana katika mabehewa ya zamani ya treni yaliyotelekezwa karibu na jiji la Thessaloniki wakielekea kufuata njia ya Balkan kuelekea Kaskazini mwa Makedonia. Kutoka kwenye mabehewa wanaruka kwenye treni za mizigo zinazowapeleka hadi Idomeni, mpakani na Macedonia Kaskazini. Wanasubiri na kuunda vikundi ili kuvuka mipaka katika milima na kufikia nchi nyingine za Ulaya kama Ujerumani, Ufaransa, Sweden nk kupitia njia ya Balkan.Picha: Nicolas Economou/NurPhoto/picture alliance

Kwenye nchi kavu, yameripotiwa kwa mfano kwenye mto Evros kwenye mpaka wa Ugiriki na Kituruki, kwenye mpaka wa Uhispania na Moroko kwenye eneo la Uhispania la Melilla, kwenye mipaka ya Poland na Belarus, Hungary na Serbia, na Kroatia-Bosnia na Herzegovina

Baharini, mamlaka za Ugiriki zimeshutumiwa kulaazimisha boti kurudi nyuma kabla ya kufika kwenye eneo la bahari la Uoma wa Ulaya. Walinzi wa pwani ya Italia pia wamedaiwa kurudisha nyuma boti kwenye bahari ya Libya.

Soma pia:Nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya zimekubalina juu ya mpango wa kuweka sheria kali za uhamiaji. 

EU pia imefikia makubaliano rasmi na Libya, na hivi karibuni na Tunisia, ikitoa fedha kwa mamlaka ili kuzuia uvukaji usio wa kawaida katika eneo la Umoja wa Ulaya kabla haujatokea.

EU inasema makubaliano hayo yananuwiwa kukabiliana na ulanguzi wa watu na kuwazuia wahamiaji kufanya vivuko vya hatari, lakini kwa Pope wa Oxfam, hivi ni sawa "vikwazo."

Ni yepi madhara kwa — kwa wale wanaorejeshwa na wanaoshtumiwa kushinikiza?

Watafuta hifadhi wanaowezekana ambao wanarudishwa nyuma wanakabiliwa na safu ya hatima, kulingana na mahali itatokea, Pope aliendelea. Huko Ugiriki, ambapo Oxfam imefanya utafiti, mara nyingi watu hujaribu kuingia EU. Wengine hufaulu, lakini wengine huishia kukwama Uturuki, alisema. Baadhi ya wale waliorudishwa nchini Libya wameripotiwa kuishia katika vituo vya kuzwuilia. "Bado tuna ripoti zinazoendelea za utumwa wa binadamu, ubakaji, mateso, unyang'anyi, ulanguzi," Pope alisema.

Kwa Hanaa Hakiki wa Kituo cha Ulaya cha Haki za Kikatiba na Kibinadamu (ECCHR), inafaa kusisitiza kwamba hakuna anayejua kwa hakika ni waomba hifadhi wangapi wameishia kufariki baada ya kufukuzwa.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya waafikiana kuhusu uhamiaji

"Kifo mara zote kilikuwa moja ya hatari itokakanayo na kurudishwa nyumba, kwa sababu kila mara urejeshaji huo hufanyika kutojali kabisaa kuhusu nini kitatokea kwa watu hawa," Hakiki aliiambia DW. ECCHR, ambayo imefungua kesi kwa idadi ya watu wanaodai kuzuiwa kinyume cha sheria kuingia EU, pia imefanya kazi na watu ambao walizuiliwa kwa siri au kuteswa wakati wa urejeshaji, alisema.

Soma pia:Umoja wa Mataifa wa ripoti ongozeko la vifo vya wakimbizi wanaovuka bahari ya Mediterian. 

Kufikia sasa, nchi zinazoshutumiwa kufukuza wahamiaji hazijakabiliwa na madhara mengi, Hakiki aliongeza. Mahakama ya Ulaya ya Haki za binadamu imeonyesha shauku kidogo juu ya malalamiko ya watu binafsi, kulingana naye, na Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya haijaanzisha kesi za kinidhamu dhidi ya nchi wanachama zinazoshutumiwa kufukuza wahamiaji hasa. Kwa kuzingatia mazingira magumu na hatarishi ya wanaotafuta hifadhi na wahamiaji, ni vigumu kwa mtu yeyote ambaye anaamini kuwa wamefukuzwa kinyume cha sheria kufungua kesi dhidi ya mamlaka, alisisitiza.

Pope wa Oxfam aliiambia DW kwamba urejeshaji unonekana kuwa wa kimfumo zaidi katika miaka ya hivi karibuni na ushirikiano na watendaji wasio wa Umoja wa Ulaya umeongezeka.

"EU kimsingi inajenga aina hii ya mtandao changamano wa sera, hatua za uendeshaji na makubaliano ya nchi ya tatu ili kuzuia watu wasiweze kudai haki ya hifadhi katika EU," alisema.

"Inageuka aina fulani ya mfumo kivuli wa hifadhi."