1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani wataka mahkama ilazimishe kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa rais Zimbabwe

Mohamed Dahman5 Aprili 2008

Chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe MDC leo kinajiandaa kwenda mahkamani kujaribu kutaka tume ya uchaguzi nchini humo ilizamishwe kutowa matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika Jumamosi iliopita.

https://p.dw.com/p/DcZk
Vtoile Silaigwana (katikati)Naibu Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe ZEC akitangaza matokeo ya uchaguzi wa bunge. Matokeo ya uchaguzi wa rais bado kutangazwa .Picha: picture-alliance/ dpa

Inaelezwa kwamba iwapo chama hicho kitafanikiwa kupata amri hiyo ya mahkama kuu matokeo hayo yanaweza kutolewa katika masaa machache.Umoja wa Ulaya ni miongoni mwa jumuiya ya kimataifa zilizotowa wito kwa tume ya uchaguzi ya Zimbabwe kutangaza matokeo hayo.Hatua hiyo ya chama cha upinzani inakuja siku moja baada ya chama tawala cha ZANU-PF kutangaza kwamba Rais Robert Mugabe atagombania duru ya pili ya uchaguzi huo wa rais dhidi ya mgombea wa chama cha upinzai cha MDC Morgan Tsvangirai.

Chama cha MDC kinadai kwamba Tsvangirai ameshinda kwa zaidi ya asilimia 50 ya kura zinazohitajika kuepusha marudio ya uchaguzi huo wa rais.

Chama hicho cha upinzani kimetaka Umoja wa Mataifa kuingilia kati kuepusha umwagaji damu katika mchuano wa marudio ya uchaguzi wa rais ambapo inahofu kwamba Rais Mugabe atatumia nguvu za kikatili zilizosababisha kuuwawa kwa mamia ya watu wakati wa chaguzi zilizopita.

Wakati huo huo chama cha ZANU-PF kimepinga matokeo ya uchaguzi wa bunge ambayo kwa mara ya kwanza kabisa kimepoteza wingi wa viti kudhibiti bunge kuwahi kushuhudiwa kwa takriban miongo mitatu.

Chama hicho kinataka kuhesabiwa upya kwa kura katika majimbo 16 ya uchaguzi.