Vyama vya upinzani nchini Tanzania vimeshindwa kwa mara nyengine na chama tawala CCM, katika chaguzi za marudio zilizofanyika Tanzania bara pamoja na visiwani Zanzibar. Mohammed Khelef, amezungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya chama cha upinzani CUF, Julius Mtatiro, akitaka kujua matokeo ya chaguzi hizi yanaashiria nini kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020?