Upinzani wa Venezuela wazidisha mbinyo wake:
6 Machi 2004Matangazo
CARACAS: Nchini Venezuela upinzani umetangazi kuwa umeandaa maandamano makubwa hii leo dhidi ya Rais Hugo Chavez. Wakati huo huo upinzani huo unafanya mapatano pamoja na tume ya uchaguzi juu ya mwito wao uliokataliwa kuwa Rais Chavez aachishwe wadhifa wake. Hapo Jumanne tume ya uchaguzi iliukataa mwito huo kufuatana na hoja kuwa hazijapatikana saini miliyoni 2.4 kama vile inavyotakiwa na sheria. Kutoka jumla ya kura miliyoni tatu zilizotolewa ni nusu tu zinakubalika, ilisema tume ya uchaguzi. Kwa mara nyingine tena Rais Chavez ameishutumu Marekani kuwa inachochea mgogoro wa siasa za ndani nchini Venezuela.