SiasaPoland
Upinzani Poland watazamiwa kupata wabunge wengi
17 Oktoba 2023Matangazo
Vyama hivyo vitatu vya upinzani kwa pamoja vina asilimia 53 huku chama tawala PiS kikiwa na asilimia 35.6 baada ya asilimia 99 ya kura zote kuhesabiwa.
Mkuu wa zamani wa Umoja wa Ulaya Donald Tusk anayeuongoza upinzani aliutaja uchaguzi huo wa ubunge uliofanyika Jumapili kuwa "nafasi ya mwisho” ya kuokoa demokrasia.
Uchaguzi huo, ulishuhudia idadi kubwa zaidi ya watu waliojitokeza kupiga kura tangu kuanguka kwa Ukomunisti.
Huenda matokeo hayo yakamaliza miaka minane ya utawala wa chama cha kizalendo cha Sheria na Haki.