1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Upinzani nchini Senegal wapingana na uamuzi wa mahakama

10 Mei 2023

Chama cha Kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko nchini Senegali kimeupinga uamuzi wa mahakama ambao unaweza kumzuia kiongozi huyo kugombea urais katika uchaguzi ujao wa mwakakani.

https://p.dw.com/p/4R7vE
Kiongozi wa chama cha upinzani Ousmane Sonko akizungumza na waandishi wa habari kutoa mwito kwa upinzani kuungana dhidi ya serikali ya Macky Sall.
Senegal iko katika misukosuko ya kisiasa iliyoliyumbisha taifa hilo katika nyanja mbalimbali.Picha: Fatma Esma Arslan/AA/picture alliance

Kauli hiyo ni majibu ya kwanza kutoka kwa upande wa Sonko kufuatia uamuzi wa mahakama wa Jumatatu wa kuongeza muda wake wa adhabu iliyositishwa katika kesi ya kashfa, kwa kiwango ambacho kinaweza kumfanya mwanasiasa huyo maarufu asiwe na haki ya kugombea katika uchaguzi wa urais wa Februari, ikiwa haitakatiwa rufaa. Senegal, ambayo ilipata uhuru kutoka kwa Ufaransa mwaka 1960, ilikuwa ikizingatiwa sana kama mfano wa demokrasia imara katika eneo la Magharibi ya Afrika, lakini sakata la muda mrefu la kisheria la Sonko na mashaka ya Rais Sall kujaribu kugombea muhula wa tatu vimechochea maandamano katika miaka ya hivi karibuni.