Israel: Upinzani wamshutumu Netanyahu kumfuta kazi Gallant
6 Novemba 2024Katiku kikao cha pamoja cha waandishi habari, wapinzani wamemtuhumu Netanyahu kwa kuyatanguliza mbele maslahi yake ya kisiasa badala ya nchi.
Netanyahu alimtimua Yoav Gallant baada ya tofauti zao za wazi kuhusu operesheni ya kijeshi ya Israel ya kulipiza shambulizi lililofanywa na wanamgambo wa Hamas dhidi ya Israel Oktoba 6 mwaka jana.
Soma pia:Netanyahu amfuta kazi waziri wake wa ulinzi Yoav Gallant
Kiongozi mkuu wa upinzani Benny Gantz, ambaye alijiondoa katika serikali ya Netanyahu mwezi Juni kwa kukosa mpango wa baada ya vita vya Gaza, amesema hatua hiyo ya Netanyahu imekuja wakati mbaya akiongeza kuwa ni "uzembe mkubwa wa kiusalama."
Uamuazi wa kumfuta kazi Gallant imejiri wakati ambao Israel inapambana kuongeza idadi ya askari, huku vikosi vya ardhini vikitumwa kukabiliana na Hamas huko Ukanda wa Gaza na Hezbollah nchini Lebanon.