SiasaVisiwa vya Comoros
Upinzani Comoro wawasilisha kesi mahakamani kupinga matokeo
20 Januari 2024Matangazo
Abdallah Mohamad Daoudou, aliyekuwa mgombea wa chama cha upinzani cha Chungwa, ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa, wanaitaka mahakama ya juu nchini humo kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais wa Januari 14.
Upinzani unadai kuwa uchaguzi huo uligubikwa na visa vya udanganyifu ikiwemo masunduku ya kura kujazwa mapema na zoezi la kupiga kura kukamilika kabla ya muda rasmi wa kufunga vituo vya kura.
Serikali hata hivyo imekanusha madai hayo.
Rais Azali Assoumani aliyekuwa akishindana na wapinzani watano, alitangazwa mshindi kwa kupata asilimia 62.97 ya kura. Upinzani umepinga matokeo hayo na kuandaa maandamano ambayo yamesababisha kifo cha mtu mmoja na kuacha watu wengine 25 na majeraha.