Upande wa upinzani nchini Ethiopia unatishia kulisusia bunge ikiwa madai yao hayatazingatiwa
24 Mei 2005Upande wa upinzani nchini Ethiopia umetishia kulisusia bunge ikiwa madai yao hayatazingatiwa.Upande wa upinzani umewataka wananchi wajiandae kwa maandamano ya amani.Vyama vya upinzani vinadai pamefanyika visa vya udanganyifu uchaguzi wa bunge ulipoitishwa may 15 iliyopita.Kamisheni kuu ya uchaguzi imetangaza matokeo ya uchaguzi toka vituo 98 vya upigaji kura.Kwa mujibu wa matokeo hayo,chama cha EPRDF na washirika wake serikalini, ,kimejipatia viti 62 na chama kikuu cha upinzani-Muungano kwaajili ya umoja na demokrasia CUD kimejikingia viti 36.Chama cha upinzani cha CUD kinasema kimetuma malalamiko kuhusu visa vya udanganyifu vilivyotokea katika vituo 139 kati ya 547 vya upigaji kura kote nchini.Wachunguzi wa kimataifa waliosimamia uchaguzi huo hawakusema chochote kuhusu visa hivyo vya udanganyifu.