1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upande wa upimnzani nchini Ethiopia unasema kuna uwezekano wa kuibuka na ushindi kufuatia uchaguzi wa ajumapili iliyopita

18 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFCH
Muungano wa vyama vya upinzani nchini Ethiopia umesema hii leo matokeo ya mwanzo ya uchaguzi wa bunge yanaashiria uwezekano wa kuibuka na ushindi.“Hali inaonyesha dhahiri kwamba muungano kwaajili ya umoja na demokrasia CUD utaibuka na ushindi,kwa kujipatia wingi wa kutosha wa viti kuweza kuunda serikali“ amesema hayo makamo mwenyekiti wa CUD Berhanu Nega mbele ya waandishi habari mjini Addis Ababa.Kiongozi huyo wa upinzani pamoja na wawakilishi wa chama cha UEDF waliohudhuria mkutano pamoja na waandishi habari wamesema kila kitu kimeweekwa tayari kuepukana na njama ya serikali kughoshi matokeo ya uchaguzi.Chama tawala cha mapinduzi ya kidemokrasi ya umma wa Ethiopia-EPRDF kimejitangazia ushindi tangu jumatatu iliyopita na serikali ya waziri mkuu Meles Zenawi ikapitisha sheria kupiga marufuku mikutano na maandamano kwa kipindi cha mwezi mmoja.