1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uongozi wa muda wa FIFA waomba mshikamano

18 Desemba 2015

Uongozi wa muda wa FIFA umetoa wito wa kuwepo imani katika Shirikisho hilo la Kandanda Duniani lililopakwa tope kutokana na kashfa kubwa ya rushwa miongoni mwa maafisa wake wakuu

https://p.dw.com/p/1HQ5M
Zürich FIFA Interims-Präsident Issa Hayatou
Picha: Getty Imgages/AFP/F. Coffrini

Taarifa iliyotolewa na kaimu rais Issa Hayatou na katibu mkuu Markus Kattner, imewaomba wanachama wote 209 wa FIFA kuunga mkono kikamilifu mpango mpana wa mageuzi ili kuutatua mgogoro uliopo kwa sasa. Viongozi hao wamesema mstakabali wa FIFA na maendelo ya kandanda vitategemea kujitolea kwa wadau wote wa FIFA.

Huku likikabiliwa na uchunguzi wa uhalifu na maafisa wa Marekani na Uswisi, kukamatwa kwa maafisa wake na kusimamishwa kazi kwa Joseph Blatter na wengine, kamati kuu ya FIFA ilipitisha mpango wa mageuzi ambao utaidhinishwa katika mkutano mkuu mnamo Februari mwakani wakati rais mpya atachaguliwa pia.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu