1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uongozi wa kijeshi Misri walivunja bunge

14 Februari 2011

Uongozi mpya wa kijeshi nchini Misri umetangaza kulivunja bunge na kusimamisha katiba, siku mbili baada ya kujiuzulu rais wa nchi hiyo, Hosni Mubarak.

https://p.dw.com/p/10GiA
Kiongozi wa kijeshi Misri, Field Marshal Mohammed Hussein TantawiPicha: picture-alliance/ZB

Katika taarifa yake, Baraza Kuu la Kijeshi jana lilisema kuwa litasimamia masuala ya nchi hiyo hadi uchaguzi mpya wa wabunge utakapofanyika.

Serikali hiyo mpya ya Misri pia ilikutana kwa mara ya kwanza, ikisema kuwa kipaumbele chake cha kwanza ni kurejesha hali ya usalama na kuwezesha maisha ya kila siku ya raia wake.

Waziri Mkuu, Ahmed Shafiq amesema hana haraka ya kuwateua mawaziri, na badala yake atafanya tu maamuzi iwapo ana imani ya kutosha katika uteuzi.

Pia Waziri huyo Mkuu wa Misri, alisema serikali itaweka kipaumbele katika kupunguza bei za vyakula, wakati ambapo mamilioni ya Wamisri wanategemea ruzuku ya serikali ili kuishi.