1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNICEF: Watoto 167 milioni wataishi katika umaskini 2030

Sylvia Mwehozi28 Juni 2016

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia watoto UNICEF, limeonya kwamba watoto walio na umri chini ya miaka 5 watafariki kutokana na sababu zinazoweza kuzuilika kati ya sasa na mwaka 2030.

https://p.dw.com/p/1JErc
Picha: picture-alliance/dpa/Unicef/Esiebo

Katika ripoti yake ya mwaka UNICEF imesema kwamba kulingana na mwenendo wa hivi karibuni na makadirio ya ukuaji wa watu, watoto milioni 167 wataishi katika umaskini uliokithiri, milioni 60 hawataweza kuhudhuria elimu ya msingi na wanawake milioni 750 watakuwa katika ndoa kama watoto ifikapo mwaka 2030, labda ikiwa suala la usawa litashughulikiwa na nchi ziharakishe jitihada za kuboresha afya na elimu kwa wasiojiweza.

Naibu mkurugenzi mtendaji wa UNICEF Justin Forsyth amesema katika uzinduzi wa ripoti hiyo na "kutuma ujumbe kwa dunia isiyo salama" hasa wahamiaji na wakimbizi ikiwa ni pamoja na mamilioni ya watoto.

Sababu zinazochangia

Wengi wanakimbia kwa sababu ya umaskini na kukosekana kwa usawa, amesema mkurugenzi huyo na kwamba sababu hizo zinaweza kushughulikiwa.

"Kazi yetu kama UNICEF ni kuwepo na kusaidia watoto kuishi" alisema Forsyth, akiongeza kwamba shirika hilo linapaswa kuhakikisha kunakuwa na mjadala mzito wa kuhusu masuala magumu na kupaza ujumbe wa kuwasaidia wasiojiweza.

Mkurugenzi wa programu UNICEF Ted Chaiban amesema katika nyongeza ya vijana wanaokimbia umaskini na kukosekana kwa usawa, pia wapo watoto zaidi wanaoishi katika maeneo ya vita karibu milioni 250 na wengine milioni 30 hawana makazi..

Mtoto akijifunza hesabu nchini Burundi
Mtoto akijifunza hesabu nchini BurundiPicha: picture alliance/dpa-Zentralbild/T. Schulze

Kwa mujibu wake, ukosefu wa usawa upo kila nchi na watoto asilimia 20 duniani maskini ya wakazi ni mara mbili ambao watafariki katika umri chini ya miaka mitano zaidi ya asilimia 20 ya watoto tajiri.

Hali ni mbaya

Ripoti hiyo inasema asilimia 80 ya vifo vinavyoweza zuilika vinatokea katika maeneo ya kusini mwa Asia na kusini mwa jangwa la Sahara, nusu ya hivyo ni katika nchi za India, Nigeria, Pakistan, Congo na Ethiopia.

UNICEF imewataka nchi wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa kubuni mipango ya kitaifa ikayowasaidia wasiojiweza na watoto walioachwa kando kwanza pamoja na kujiwekea malengo maalumu ya kupunguza pengo kati ya maskini na tajiri.

Ripoti hiyo inaona kwamba karibu watoto milioni 147 walio na umri wa mwaka mmoja hadi mitano wanaweza kuokolewa kutokana vifo kwa kuongeza matumizi ya asilimia 2 tu katika nchi 74.

UNICEF imesema pia kwamba ina ushahidi wa kila dola moja inayotumika katika chanjo kwa watoto wasiojiweza inaweza kuzalisha dola 16 katika suala la faida za kiuchumi.

Kulingana na " Ripoti ya Hali ya Watoto Duniani 2016, " fedha za uhamisho zimesaidia watoto kukaa katika shule kwa muda mrefu na kwa wastani, kila mwaka wa elimu , mtoto anapata ongezeko la mapato ya mtu mzima kwa asilimia 10 .

Mwandishi: Sylvia Mwehozi/AP

Mhariri: Mohammed Khelef