1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNHCR yaikosowa Ghana kuwarejesha waomba hifadhi

13 Julai 2023

Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limesema lina wasiwasi na ripoti za waomba hifadhi wanaowasili nchini Ghana kurejeshwa makwao.

https://p.dw.com/p/4TqwL
Ghana | Wachen gegen Extremisten an den Grenzen zu Togo und Burkina Faso
Picha: Benita Kyaw/DW

Mamia ya wakimbizi kutoka nchi jirani ya Burkina Faso wamekuwa wakikimbilia nchini Ghana kuomba hifadhi.

Burkina Faso ni mojawapo kati ya nchi za Afrika Magharibi ambazo zinakabiliana na makundi yenye silaha.

Makundi hayo yaliyokita mizizi kaskazini mwa Mali yanadhibiti ardhi katika eneo hilo tangu muongo mmoja uliopita na yamesababisha vifo vya maelfu ya watu.

Soma zaidi: Burkina yaipongeza Mali kwa kulitaka jeshi la UN kuondoka nchini

UNHCR imeirai serikali ya Ghana kuhakikisha kuwa inawapatia hifadhi raia wa Burkina Faso wanaokimbia ghasia na kusitisha hatua za kuwarejesha walikotoka.

Zaidi ya watu milioni 2 wameyakimbia makaazi yao nchini Burkina Faso.

Wanawake wengi na watoto wametafuta hifadhi kaskazini mwa Ghana ambako pia machafuko yamepamba moto katika miaka ya hivi karibuni.