1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNDP: Kusini mwa jangwa la Sahara ni kituo cha itikadi kali

7 Februari 2023

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa,UNDP, eneo la kusini mwa jangwa la Sahara sasa limekuwa kituo kikuu kipya cha itikadi kali, ambapo watu wanazidi kujiunga na makundi ya magaidi.

https://p.dw.com/p/4NCJ3
Logo UNDP United Nations Development Programme

Ripoti ya shirika la UNDP imesema asilimia 92 ya watu wapya wamejiunga na makundi hayo kwa ajili ya kujipatia riziki za maisha kulinganisha na sababu zilizotajwa hapo awali katika ripoti ya mwaka 2017.

Asasi hiyo imeeleza katika ripoti yake kwamba maisha ya watu wengi barani Afrika yameathirika kwa kiwango kikubwa kutokana na maambukizi ya Covid-19, mfumuko wa bei na mabadiliko ya tabia nchi. Watu wapatao 2200 walihojiwa kwenye nchi nane za Afrika kwa ajili ya ripoti hiyo.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limefahamisha katika ripoti yake kwamba mashambulio ya kigaidi yapatayo 4,155 yameorodheshwa tangu mwaka 2017 barani Afrika kote. Watu zaidi ya 18,000  waliuawa kutokana na mashambulio hayo, idadi kubwa ikiwa nchini Somalia.

Asasi ya UNDP imependekeza kuboreshwa kwa huduma za msingi na kuleta maisha mazuri ili kuwazuia watu kujiunga na makundi ya magaidi.