Unaujua uwanja wa ndege mkubwa zaidi duniani?
Istanbul itakuwa na uwanja mpya wa ndege, ambao Uturuki inasema utakuwa mkubwa zaidi duniani. Lakini je hili ni kweli? DW inaangazia viwanja vingine vikubwa duniani.
Hartsfield-Jackson Airport, Atlanta, US
Linapokuja suala la idadi ya abiria, hakuna uwanja wa ndege unaoweza kufananishwa na uwanja huu uliopo Atlanta. Karibu watu milioni 104 walipitia uwanja wa Hartsfield-Jackson mwaka 2017, hii ikiwa ni kulingana na takwimu zilizotolewa na shirika la viwanja vya ndege ACI. Hakuna uwanja wa ndege mwingine uliofikia rekodi hiyo. Hii inafanya Hartsfield-Jackson kuongoza kwenye orodha yetu.
Beijing Capital International Airport, China
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital ni wa pili kwa kuchukua idadi kubwa ya abiria, ulichukua watu milioni 95.8 mwaka 2017. Uwanja huo wa ndege ulijengwa kabla ya michezo ya Olimpiki ya 2008. Mtaalamu wa michoro kutoka Uingereza Norman Foster aliandaa mchoro wa uwanja mpya wa ndege na unaovutia kwa ajili ya tukio hilo.
Dubai International Airport
Mwaka 2017, uwanja wa ndege wa Dubai ulipokea abiria milioni 88. Karibu abiria wote hawakuwa Waarabu - karibu abiria milioni 87.72. Wengi wao wanaonekana kuufahamu uwanja wa kimataifa wa Dubai kwa sifa yake ya kuwa na maduka mengi unayoweza kufanya manunuzi mbalimbali.
Tokyo Haneda Airport, Japan
Alas, uliopo katika mji mkuu wa Japan, si miongoni mwa viwanja vitatu vikubwa vinavyoongoza, lakini uwanja huu unapokea wasafiri milioni 85.4 kwa mwaka. Idadi hii inatosha kabisa kwa uwanja huu kushika nafasi ya nne katika orodha yetu.
Los Angeles International Airport, US
Kama unakwenda likizo jijini California huko Marekani, basi kuna uwezekano mkubwa wa kushukia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Los Angeles, unaojulikana zaidi kama LAX. Mzunguko wa abiria haufikii hata kidogo uwanja wa ndege wa Atlanta, lakini hata hivyo bado ulikuwa na wageni zaidi ya milioni 85.5 mwaka jana.
O'Hare International Airport, Chicago, US
Hata huko Chicago, huwa hakuna mapumziko kuanzia kwa mashabiki wa nyota wa soka wa Ujerumani Bastian Schweinsteiger. Mchezaji huyo wa zamani wa Bayern Munich na Manchester United sasa anachezea Chicago Fire, na mara nyingi hupitia O'Hare. Schweinsteiger ni mmoja tu wa wasafiri milioni 79.81 ambao hupitia Chicago, kiwanja kilichopewa jina la rubani wa vita vya pili vya dunia, raia wa Marekani.
London Heathrow, UK
London ina viwanja vya ndege vitatu, na kikubwa zaidi na kinachojulikana sana ni Heathrow. Huhudumia abiria zaidi ya milioni 78 kwa mwaka. Na kina uwezo wa kuwahudumia abiria hao wote kikiwa na njia mbili tu kwenye uwanja wake.
Hong Kong International Airport, China
Huna budi kuwa katika ndege ili kuona kwa uzuri kabisa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hong Kong, ambao wenyeji wanauita Chek Lap Kok. Uwanja huu huvutia sana na uliweza kuhudumia abiria milioni 72.67 kwa mwaka 2017. Hong Kong au "bandari yenye harufu nzuri" kwa lugha ya Kiingereza, umejengwa kwenye ardhi iliyohifadhiwa katika kisiwa cha Chek Lap Kok kwenye Bahari ya Kusini ya China.
Shanghai Pudong International Airport, China
Usalama kwanza! Ni moja ya viwanja vya ndege vikubwa vya Shanghai vilivyo nyuma ya kile cha Hong Kong. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Pudong ulihudumia abiria milioni 70 mwaka 2017. Idadi hii inaonyesha kushuka kidogo kutoka mwaka uliopita, lakini ndege za mizigo zilibeba mizigo kwa zaidi ya asilimia 11, hii ikiwa ni kulingana na ACI.
Paris-Charles de Gaulle, France
Uwanja wa ndege wa Paris uliopewa jina la Rais de Gaulle, pia unajulikana kwa jina la Roissy, unashika nafasi ya 10 kwenye orodha yetu ya viwanja vilivyo na shughuli nyingi zaidi duniani. Mwaka jana, ulipokea wageni milioni 69.47. Lakini takwimu hizo sio kila kitu kwa kuangazia nafasi ya uwanja huo; kuna pia vigezo kama kiasi cha bidhaa zinazosafirishwa, ukubwa, namba ya vituo na mengine mengi.
Berlin-Brandenburg Airport, Germany
Ni hakika huchukua muda mrefu kujenga uwanja wa ndege. Ni kwa maana hiyo basi, Wajerumani wanaweza kushika nambari 1. Labda ni suala la ufafanuzi tu: Miaka tisa ambayo imepita sasa tangu ujenzi huo ulipoanza inaweza kuchukuliwa kama kigezo cha ukamilifu.