Baraza la Usalama UN kupigia kura azimio juu Gaza Jumatatu
23 Machi 2024Hatua hiyo imechukuliwa ili kutoa fursa ya majadiliano zaidi. Awali rasimu hiyo ilikusudiwa kupigiwa kura leo Jumamosi.
Rasimu hiyo mpya inataka usitishwaji wa mara moja wa mapigano katika mwezi mtukufu unaoendelea wa Ramadhan na kisha baadaye yapatikane makubaliano ya kusitisha kabisa mapigano.
Wanachama wanane kati ya 10 wasio wa kudumu wa baraza hilo wamekuwa wakifanyia kazi rasimu hiyo, ambayo pia inataka kuachiliwa huru "mara moja na bila masharti" mateka wote waliochukuliwa na Hamas pamoja na kuondolewa kwa "vizuizi vyote" kwa misaada ya kibinadamu kuingia kwenye Ukanda wa Gaza.
Soma pia:Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lashindwa kupitisha azimio la kusitisha mapigano Gaza
Rasimu hiyo mpya inafuatia kushindwa kwa azimio lililopendekezwa na Marekani hapo jana Ijumaa. Urusi na China zilitumia kura za turufu kulipinga azimio hilo ambalo pia lilikataliwa na mataifa ya Kiarabu.