1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGuatemala

UN yasikitishwa na jaribio la kubalisha uchaguzi Guatemala

9 Desemba 2023

Kamishna Mkuu wa Ofisi ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa, Volker Turk, amechukizwa na majaribio ya kudhoofisha matokeo ya uchaguzi wa Guatemala na kutaka matakwa ya wapiga kura kuzingatiwa.

https://p.dw.com/p/4ZyGk
Kairo UN-Menschenrechtskommissar Türk
Picha: KHALED DESOUKI/AFP

Mgombea anayepinga ufisadi Bernardo Arevalo ambaye anatazamiwa kushika wadhifa huo Januari 14 amekabiliwa na changamoto nyingi za kisheria tangu ushindi wake wa kushangaza wa duru ya pili mwezi Agosti, ikiwa ni pamoja na majaribio ya kukisimamisha chama chake cha Semilla na kumzuia kuchukua madaraka.

Siku ya Ijumaa, mwendesha mashtaka Leonor Morales alisema uchunguzi umehitimisha kwamba uchaguzi wa Arevalo, makamu wake wa rais na wabunge ulikuwa "batili " kutokana na makosa yaliyofanyika wakati wa kuhesabu kura.

Turk, amezitaka mamlaka za Guatemala kuhifadhi na kuheshimu haki zote za binadamu, ikiwa ni pamoja na uhuru wa kujieleza na uhuru wa kukusanyika kwa amani wakati wote.