1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yalaani hukumu ya miaka 15 ya mwandishi Libya

3 Agosti 2020

Umoja wa Mataifa nchini Libya umezungumzia kutoridhishwa kwake na hatua ya kufungwa miaka 15 jela kwa mwandishi wa habari mashariki mwa nchi hiyo, eneo linalodhibitiwa na mbabe wa kivita Khalifa Haftar.

https://p.dw.com/p/3gKYN
UN-Sicherheitsrat New York 2016 | Waffenembargo Libyen
Picha: Imago Images/Xinhua

Katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter Umoja wa Mataifa umesema hukumu hiyo inakiuka sheria za Libya pamoja na jukumu lake la kimataifa la kutoa maamuzi ya haki na uhuru wa kujieleza.

Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Libya Alan Bugeja amesema ana wasiwasi mkubwa hasa kutokana na hukumu hiyo hasa kwa kuwa mwandishi huyo alikuwa kizuizini kwa zaidi ya miaka miwili.

Uongozi mashariki mwa Libya haujaweka wazi hasa mashtaka yaliyokuwa yanamkabili mwandishi huyo, ila vyombo vya habari nchini humo vinasema alituhumiwa kwa kuwasiliana na mashirika yaliyopigwa marufuku katika eneo hilo la Libya.