1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Mzozo wa Sudan uwe funzo kwengineko

2 Agosti 2023

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Nicholas Haysom amesema mgogoro wa Sudan unapaswa kutumiwa kama funzo na kuitaka nchi hiyo kuweka msingi wa kuandaliwa kwa uchaguzi huru mwaka ujao.

https://p.dw.com/p/4UhEE
Tschad Flüchtlinge aus Sudan Darfur
Picha: ZOHRA BENSEMRA/REUTERS

Hayson ameihimiza Sudan Kusini kuimarisha misingi ya amani, utulivu na utawala unaoshirikisha kila upande.Umoja wa Mataifa umeukosoa mara kwa mara uongozi wa Sudan Kusini kwa kuchochea ghasia, kukandamiza uhuru wa kisiasa na kupora mali ya umma.Rais Salva Kiir ameapa kuwa nchi hiyo itafanya uchaguzi wa kwanza kabisa wa urais mnamo Desemba mwaka 2024, japo mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuwa mamlaka inapaswa kuchukua hatua za haraka kuweka mazingira mazuri ya kufanyika uchaguzi kwa njia huru na haki.Tangu ilipojinyakulia uhuru wake kutoka Sudan mwaka 2011, nchi hiyo mpya zaidi duniani imekabiliwa na mizozo ikiwemo vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimegharimu maisha ya watu 400,000 kabla ya kusainiwa mkataba wa amani mwaka 2018.