UN: Mashambulizi kwa Ukraine yazidisha ugumu wa maisha
7 Desemba 2023Matangazo
Hali hiyo inatokea katika kipimndi hiki cha majira ya baridi kali na theluji. Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Miroslav Jenca ameliambia Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa kwamba mashambulizi ya Urusi kila siku dhidi ya miundombinu ya kiraia nchini Ukraine yamesababisha vifo vya raia. Amesema Urusi hivi karibuni imezidisha mashambulizi yake katika maeneo yenye watu wengi ikiwa ni pamoja na mji mkuu, Kyiv. Kulingana naShirikala Kimataifa la Nishati ya Atomiki, tangu Urusi ilipoivamia Ukraine, umeme ulikatika kwa mara ya nane kwenye kiwanda cha Zaporizhzhia ambacho ni kikubwa zaidi barani Ulaya.