Makubaliano ya ulinzi wa bahari na viumbe yafikiwa Panama
5 Machi 2023Matangazo
Hatua hiyo imefikiwa jana usiku baada ya mkutano wa kina wa saa takriban 40 uliofanyika huko Panama. Kufikiwa makubaliano hayo kunamaliza miaka 15 ya mivutano kuhusu suala hilo.
Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametowa taarifa hiyo akisema ni muhimu kushughulikia migogoro mitatu ya dunia ambayo ni mabadiliko ya tabia nchi,uchafuzi wa mazingira na kuangamia kwa bayoanuai.
Lengo kuwa la msingi la mkutano wa Panama, lilikuwa ni kushughulika kuelekea kufikia hatua ya kutenga alau asilimia 30 ya eneo la bahari kuu litakalowekewa ulinzi maalum.
Hatua iliyofikiwa imepongezwa na mashirika ya wanaharakati wa mazingira waliotaka sasa utekelezaji wa haraka ufanyike.