UN: Mahala pa hatari zaidi kwa wanawake ni nyumbani
25 Novemba 2024Mashirika hayo mawili ya Umoja wa Mataifa yamesema kimataifa, mpenzi au mwanafamilia alihusika kwa vifo vya takriban wanawake na wasichana 51,100 mwaka 2023, ongezeko kutoka takriban waathiriwa 48,800 mwaka 2022.
Mataifa yatoa data zaidi ya ukatili dhidi ya wanawake
Ripoti hiyo iliyotolewa leo ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake, imesema ongezeko hilo kwa kiasi kikubwa linatokana na kupatikana kwa data zaidi kutoka kwa mataifa na sio mauajizaidi.
Lakini mashirika hayo mawili yamesisitiza kuwa wanawake na wasichana kila mahali wanaendelea kuathirika na aina hii ya ukatili wa kijinsia uliokithiri na kwamba hakuna eneo lililo salama.
Ukatili dhidi ya wanawake uliongezeka Ujerumani mwaka 2023
Ripoti hiyo pia imesema, idadi kubwa zaidi ya mauaji yanayofanywa na wapenzi wa karibu na familia ilikuwa barani Afrika na kiwango cha wastani cha waathiriwa 21,700 mnamo mwaka 2023.
Afrika yaongoza katika ukatili dhidi ya wanawake
Afrika pia ilikuwa na idadi kubwa zaidi ya waathiriwa ikilinganishwa na ukubwa wa idadi ya watu wake, kiwango kikiwa waathiriwa 2.9 kwa kila watu 100,000.
Ripoti hiyo imeendelea kusema pia kulikuwa na viwango vya juu mwaka jana vya waathiriwa wanawakekatika maeneo ya Amerika ambapo vilikuwa 1.6 kwa kila wanawake 100,000 na katika kanda ya Oceania kiwango kilikuwa waathiriwa 1.5 kwa 100,000.
Maelfu waandamana kulaani dhulma dhidi ya wanawake
Viwango vilikuwa chini sana barani Asia ambayo ilikuwa na waathiriwa 0.8 kwa wanawake 100,000 na Ulaya kwa 0.6 kwa wanawake 100,000.
Kulingana na ripoti hiyo, mauaji ya kukusudia ya wanawake katika maeneo ya faragha barani Ulaya na Amerika, kwa kiasi kikubwa yalitekelezwa na wapenzi wa karibu.
Ujerumani inakabiliwa na tatizo la ukatili dhidi ya wanawake
Katika mahojiano na shirika la habari la dpa ya Siku hii ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake, waziri huyo wa masuala ya familia wa Ujerumani Lisa Paus, amesema kwamba karibu kila siku kuna tukio la mauaji ya wanawake ambayo yanaoongeza ufahamu kuhusu tatizo hilo.
Paus ameongeza kuwa kila siku, takriban wanawake 400 huathirika kutokana na ukatili wa kinyumbani.
Maandamano na hafla mbali mbali zimepangwa katika miji kadhaa nchini Ujerumani kushinikiza kusitishwa kwa ukatili dhidi ya wanawake.
Paus ataka kuwepo kwa sheria dhidi ya ukatili wa wanawake
Paus pia ametaka kufanyika kwa mabadiliko pamoja na sheria ya kusaidia kukomeshwa kwa ukatili huo ili kuwezesha kuweko kwa haki ya ulinzi na ushauri kwa wale wote walioathirika kutokana na ukatili wa kijinsia pamoja na ule wa kinyumbani.
Utafiti: Idadi ya wanawake wanaouwawa yaongezeka Tanzania
Waziri huyo ameongeza kuwa anaendelea kushinikiza uungwaji mkono wa sheria hiyo ya kupinga ukatilidhidi ya wanawake kutoka kwa vyama vyote vya kisiasa kwa ushirikiano na wizara nyingine, serikali za majimbo na mashirika.
Kupitisha sheria hiyo katika bunge la kitaifa la serikali ya shirikisho ama baraza la chini la bunge, kunahitajika uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa upinzani wa kihafidhina.