UN: Kuzama baharini ndio chanzo kikuu cha vifo vya wahamiaji
26 Machi 2024Matangazo
Shirika la IOM inasema idadi ya waliozama baharini imepindukia 36,000. Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linasema kati ya vifo 64,000 vya wahamiaji vilivyorekodiwa katika mwongo mmoja uliopita, karibu asilimia 60 vilihusishwa na kuzama. Kati ya vifo hivyo vya baharini, 27,000 vilitokea katika Bahari ya Mediterenia, njia ambayo imekuwa ikitumiwa na wahamiaji wengi wanaojaribu kufika kusini mwa Ulaya kutoka kaskazini mwa Afrika.
IOM lakini limesisitiza kwamba idadi hiyo iliyochapishwa katika ripoti hiyo haijakamilika.