1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAfghanistan

UN kufanya mazungumzo na Taliban kuhusu wanawake

5 Aprili 2023

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan utafanya leo mazungumzo na maafisa wa Taliban kutafuta ufafanuzi kuhusu marufuku mpya inayowazuia wanawake kulifanyia kazi shirika hilo la kimataifa, kote nchini humo.

https://p.dw.com/p/4PiVN
Wanawake wa Kiafghani wakisuka mazulia
Tangu kundi la Taliban lilipochukua hatamu za uongozi nchini Afghanistan, wanawake wamewekewa vizuizi vingi.Picha: ToloNews

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric amesema UNAMA imepokea ujumbe wa amri kutoka kwa watawala wa Taliban inayowapiga marufuku wafanyakazi wa kike wa Umoja wa Mataifa kufanya kazi.

Amesema hakuna agizo la maandishi lililopokelewa, lakini watafanya mikutano leo mjini Kabul ili kutafuta ufafanuzi.

Tangu wamechukua madaraka Agosti 2021, maafisa wa Taliban wameweka msururu wa vikwazo kwa wanawake wa Kiafghanistan, ikiwemo kuwapiga marufuku kupata elimu ya juu na kufanya kazi nyingi za kiserikali.

Umoja wa Mataifa huwaajiri karibu wanawake 400 wa Kiafghanistan.