UN kuendelea kutoa usaidizi kufadhili miradi ya wakimbizi
15 Novemba 2021Mratibu mkazi wa Umoja wa mataifa nchini Tanzania ndugu Zlatan Milisic ametoa ahadi hiyo mkoani Kigoma baada ya kutembelea na kukagua miradi inayofadhiliwa na mpango wa pamoja unaofahamika kwa jina la Kigoma Joint Program.
Milisic ameitaja miradi ya kipaumbele itakayopata ufadhili kuwa ni uwezeshaji vijana na wanawake kiuchumi, kupinga ukatili, huduma za maji, mazingira, kilimo na afya.
Miradi hiyo ya kimkakati inaratibiwa na umoja wa mataifa na ufadhili wake unatoka Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, kupitia mashirika 16 ya umoja wa mataifa.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu amesema uwepo wa miradi inayosimamiwa na jumuia ya Ulaya kupitia mashirika 16 ya umoja wa mataifa umewezesha kuboresha huduma za afya kwa wananchi pamoja na kupunguza umasikini kwa vijana na wanawake.