1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUswisi

Idadi ya watoto wanaochomwa chanjo yaongezeka

18 Julai 2023

Umoja wa Mataifa unasema idadi ya watoto wanaochomwa chanjo za kawaida inaongezeka tena baada ya kushuka pakubwa wakati wa janga la Uviko-19.

https://p.dw.com/p/4U2aO
Kampeini ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Polio katika eneo la Kiamako jini Nairobi nchini Kenya
Kampeini ya utoaji chanjo ya polio jijini NairobiPicha: Simon Maina Getty Images/AFP

Mkuu wa chanjo katika Shirika la Afya Duniani WHO Kate O'Brien, lakini, ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa bado kuna mapungufu makubwa yaliyo na hatari.

Mkuu wa WHO asema takwimu zilizotolewa zinatia moyo

Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebrayesus amekubaliana na hayo na kusema takwimu hizo zilizotolewa zinatia moyo. Ghebreyesus lakini ameonya kwamba wastani wa takwimu za dunia na kikanda hazitoi picha kamili na zinafunika tofauti za usawa zilizopo.

Licha ya takwimu hizo, watoto milioni 20.5 walikosa kuchomwa chanjo moja au zaidi za kawaida mwaka 2022.