1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umwagaji damu waendelea Haiti:

21 Februari 2004
https://p.dw.com/p/CFgT

PORT-AU-PRINCE. Nchini Haiti vinaendelea kupamba moto vita vya ndani vya umwagaji damu. Watu wawili walipigwa risasi na kuuawa na wengine 20 walijeruhiwa yalipotokea mapigano kati ya wafuasi na wapinzani wa Rais mtawala Jean-Bertrand Aristide katika mji mkuu Port-Au-Prince, kiliarifu Chama cha Msalaba Mwekundu. Wanadiplomasia wa nchi kadha wamemkabidhi Rais Aristide mpango wa amani. Mpango huo wa amani unashauri kuwa wanamgambo wa kiasi wapokonywe silaha na ateuliwe Waziri Mkuu mpya mwenye madaraka makubwa zaidi. Hata hivyo, inasemekana mpango huo hauna nafasi nzuri za kufanikiwa kwa sababu upinzani unashikilia ajiuzulu Rais Aristide. Na UM umesema unazidi kutiwa wasi wasi na vita hivyo vya ndani nchini Haiti.