Bar code ama msimbomilia zinazotumika kwenye bidhaa kuruhusu kuingia kwenye soko la kitaifa na kimataifa. Fatma Kange Saleh, mkuu wa taasisi ya kusimamia bar code amezungumza na DW na anashiriki kwenye makala ya Wanawake na Maendeleo kuonyesha kwamba wanawake wakipata fursa ya kuongoza huzichangamkia.