1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU Ungarn

Sekione Kitojo18 Januari 2012

Hangury imeingia matatani na umoja wa Ulaya kwa kupitisha sheria zinazoonekana kuwa zinakiuka haki za binadamu, kwa misingi ya umoja huo.

https://p.dw.com/p/13lEF
President of the Commission Jose Manuel Barroso delivers a speech after a meeting of the Commission at the European Parliament in Strasbourg eastern France, to decide whether to launch a legal challenge against Budapest over the constitution, Tuesday, Jan 17, 2012. The European Commission says it is launching legal challenges against Hungary's new constitution for violating EU laws on the independence of the national central bank and data protection agency and reducing the retirement age of judges. (Foto:Cedric Joubert/AP/dapd)
Rais wa halmashauri ya umoja wa Ulaya Jose manuel BarrosoPicha: dapd

Halmashauri ya umoja wa Ulaya imekwishatumia mbinu kadha dhidi ya serikali ya Hungary ambayo inakiuka sheria za umoja huo. Hivi sasa inahusu suala la benki kuu, mamlaka inayokusanya takwimu na mahakama. Halmashauri ya Ulaya inahisi kuwa uhuru wa vyombo hivyo vitatu unahatarishwa , kutokana na sheria iliyopitishwa hivi karibuni na utawala wa waziri mkuu Viktor Orban.

Rais wa halmashauri ya umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso jana mchana amesema kuwa tulitarajia kuwa utawala wa Hungary itafanya mabadiliko ya haraka, na kuheshimu hatua za umoja wa Ulaya za kulinda haki. Hilo halijafanyika hadi sasa.

Waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban leo Jumatano atahudhuria kikao cha bunge la Ulaya mjini Straßburg ambapo kutakuwa na mjadala kuhusu hali nchini mwake. Haya yameelezwa na rais wa bunge hilo Martin Schultz jana. Wakati huo huo waziri wa mawasiliano wa Hungary Zoltan Kovac amedokeza kuwa kuna uwezekano wa kubadilisha.

Hungarian Prime Minister Viktor Orban smiles as he briefs the media after he met with President of the Hungarian National Bank, the central bank, Andras Simor (unseen) in his office in the Parliament building in Budapest, Hungary, 06 January 2012. After the meeting Orban said he agreed with Simor on the closest possible cooperation between the government and the central bank to strengthen the confidence in the Hungarian currency forint the rate of which had reached record depth against major international currencies recently due to uncertainties about Hungary's eventual credit agreement with IMF. EPA/TAMAS KOVACS HUNGARY
Waziri mkuu wa Hungary Viktor OrbanPicha: picture-alliance/dpa

Tumesema katika siku chache zilizopita na wiki kuwa tutalishughulikia suala hili kwa mtindo wa Ulaya, na mtindo wa Kiulaya ni kwamba wakati una aina ya fikira ama unafikia katika wakati ambapo suala la kisheria halilingani na sheria za Ulaya , kwa hiyo inabidi kubadilishwa.

Iwapo Hungary haitatimiza sharti la halmashauri ya umoja wa Ulaya , itafikishwa katika mahakama ya Ulaya pamoja na kupewa adhabu ya malipo ya fedha. Hii pia itahusu kuzuiwa kwa majadiliano kati ya hungary na umoja wa Ulaya pamoja na shirika la fedha la kimataifa kuhusu msaada wa fedha, kwa kuwa umoja wa Ulaya unatilia shaka uhuru wa benki kuu ya nchi hiyo.

Umoja wa ulaya umeongeza mbinyo wake kwa Hungary pamoja na waziri mkuu wake Viktor Orban. Msemaji wa halmashauri ya umoja wa Ulaya Pia Ahrenkilde Hansen amesema kuwa , umoja wa Ulaya unataka kuthibitisha ni umbali kiasi gani Hungary iko tayari kubadilisha sheria hizo.

Bila ya kutoa hukumu mapema , matokeo ya mwisho ya tathmini hii, ni kwamba halmashauri inataka kutumia uwezo wake wote kutathmini uhusiano wa sheria za kitaifa na za umoja wa Ulaya na una haki ya kuchukua hatua yoyote ambayo itaonekana kuwa sahihi, ikiwa na maana ya uwezekano wa kuanzisha hatua za ukiukaji wa sheria katika kifungu cha 258 cha mkataba wa ulaya.

Mwaka mmoja uliopita , mwanzoni mwa uongozi wake nchini Hungary , Orban amezusha mvutano mkubwa katika bunge kutokana na kuanzisha sheria mpya za vyombo vya habari nchini humo.

Mwandishi : Christoph Hasselbach / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri : Hamidou Oummilkheir

Link: http://www.dw-world.de/dw/article/0,,6699979,00.html