Umoja wa Ulaya waongeza shinikizo dhidi ya Gbagbo
30 Desemba 2010Umoja wa Ulaya umeimarisha shinikizo la kumtaka rais Laurent Gbagbo wa Ivory Coast aondoke madarakani.
Kwa mujibu wa taarifa ya tume ya Umoja huo, idadi ya watu wa Gbagbo waliopigwa marufuku kuingia katika nchi za Umoja huo itaongezeka kutoka 19 na hadi 61.
Wakati huo huo wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imearifu kuwa Umoja wa Ulaya utawatambua wajumbe wa kiongozi wa upinzani Alassane Outtara kuwa wawakilishi wa Ivory Coast.Jumuiya ya kimataifa inamtambua bwana Outtara kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika nchini Ivory Coast mwezi novemba.
Wakati huo huo jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi Ecowas imearifu kuwa wiki ijayo itachukua hatua zaidi ili kujaribu kuleta suluhisho la mgogoro wa kisiasa unaoikabili Ivory Coast.
Hapo jumanne ujumbe wa marais watatu kutoka jumuiya ya Ecowas ulishindwa kumshawishi Gbagbo aondoke madarakani.