SiasaIsrael
Umoja wa Ulaya walaani machafuko Mashariki ya Kati
8 Aprili 2023Matangazo
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borell amesema Ulaya inakosoa vikali matendo hayo ya kikatili na kuzitaka pande zote kusitisha maramoja makabiliano pamoja na kujizuia kutanua uhasama.
Wasiwasi wa kuzuka mapigano eneo la Mashariki ya Kati unaongezeka tangu kutokea shambulizi la bunduki lilowaua raia wawili wenye nasaba ya Israel huko Ukingo wa Magharibi na shambulizi jingine kumuua mtaalii wa kitaliana mjini Tel Aviv.
Matukio hayo yamejiri baada ya polisi ya Israel kupambana na Wapalestina mnamo siku ya Jumatano ndani ya msikiti wa Al-Aqsa mjini Jerusalem.