1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBelarus

EU yakubali kuchukua hatua za vikwazo vikali kwa Belarus

26 Julai 2023

Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zimekubali kuchukua hatua za vikwazo vikali kwa Belarus pamoja na nchi hiyo kuhusika kwake katika mzozo wa Urusi na Ukraine.

https://p.dw.com/p/4UQca
Rais wa Belarus Alexander Lukashenko
Rais wa Belarus Alexander Lukashenko Picha: Alexander Zemlianichenko/AP/picture alliance

Uhispania ambayo ni rais wa kupokezana wa Umoja wa Ulaya imetoa tamko hilo leo hii Jumatano. Mabalozi wa nchi za Umoja wa Ulaya wamekubaliana kwa kauli moja juu ya hatua hizo kali kwa kuzingatia hali ya Belarus na ushiriki wa nchi hiyo katika uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Hatua hizo ni pamoja na kuwaweka kwenye orodha ya vikwazo watu binafsi na taasisi umesema Umoja wa Ulaya katika tamko lake lililochapishwa mtandaoni.