Umoja wa Ulaya wajizatiti zaidi juu ya wahamiaji haramu
18 Oktoba 2024Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana jana Alhamisi kutumia uwezo wao wote, ikiwa ni pamoja ni kuongeza misaada na kubadilisha sera ya uhamiaji ili kuharakisha zoezi la kuwarudisha wahamiaji wanaoingia kinyume cha sheria barani ulaya.
Akizungumzia suala hilo, Rais wa Kamisheni ya Ulaya, Ursula von der Leyen, amesema..
"Leo tunaona kwamba katika wale wote ambao hawana haki ya kukaa katika Umoja wa Ulaya, ni 20% tu ya wale ambao wana uamuzi wa kurejea ndio wanarudishwa katika nchi zao za asili. Kwa hiyo tunafanya kazi ili kuboresha uendeshaji na sisi hivi karibuni tutawasilisha pendekezo jipya. Pendekezo la kisheria tulilokuwa nalo toka 2018 limekwama katika Bunge na Baraza. Kwa hivyo tutakuja na pendekezo jipya kwa mara nyingine.", alisema Von der Leyen.
Uhamiaji ni mada nyeti katika nchi zote 27 wanachama wa Umoja huo. Wahamiaji 250,000 waliingia Ulaya mwaka uliopita ingawa mwaka huu idadi yao imepungua.