1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya waitahadharisha Mali kuhusu mamluki wa Urusi

21 Septemba 2021

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell ameitahadharisha Mali kwamba uhusiano wake na umoja huo huenda ukapata athari kubwa ikiwa nchi hiyo itaruhusu mamluki wa Urusi kuendesha shughuli zao nchini Mali.

https://p.dw.com/p/40c2c
USA New York | Pressekonferenz Josep Borrell
Picha: David Dee Delgado/REUTERS

Duru za kidiplomasia na ulinzi zimeliambia shirika la habari la Reuters kwamba utawala wa kijeshi nchini Mali unakaribia kuipa jukumu kampuni ya ulinzi wa kijeshi ya Wagner kupeleka mamluki watakaotoa mafunzo kwa jeshi la Mali na kuwalinda maafisa wake.

Borrell ametoa tahadhari hiyo jana ambapo pia mawaziri wa

mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya walijadiliana kuhusu suala hilo katika kikao cha faragha kilichofanyika pembezoni mwa mkutano wa viongozi wa dunia wa hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Ufaransa imeanzisha juhudi za kidiplomasia za kuzima hatua hiyo ya Mali.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW