1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya waimwagia Misri kitita cha msaada wa kifedha

12 Aprili 2024

Umoja wa Ulaya umetangaza kuipatia Misri kitita cha dola bilioni 1 kama msaada wa kifedha kwa kipindi kifupi kuusaidia uchumi wa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4ehtp
Misri | Fattah al-Sisi
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi Picha: Egyptian President Office/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Euro bilioni 4 zitatolewa katika kipindi cha kati ya mwaka 2024 hadi 2027 lakini zitasubiri kwanza idhini kutoka mataifa yote 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Mwezi uliopita Misri iliridhia kutanua mpango wa uokozi wa kiasi dola bilioni 8 zitakazotolewa na shirika la fedha la kmataifa IMF pamoja na mkataba wa kifedha na Umoja wa Ulaya ambao sehemu ya kitita chake imetangazwa hii leo. 

Misri kupokea awamu ya kwanza ya mkopo wa IMF uliopanuliwa wiki ijayo

Malengo ya msaada huo ni kupunguza ukata unaoikabili Misiri na mahitaji mengine hasa yaliyojitokeza baada ya kuzuka kwa vita vya Ukanda wa Gaza, hujuma za kundi la waasi wa Houthi na athari za vita vya Urusi na Ukraine. Pia unalenga kupunguza wimbi la uhamiaji wanaovuka bahari kuingia Ulaya kupitia ardhi ya Misri. 

Umoja wa Ulaya umesema msaada huo unafungamanishwa na masharti kwa Misri kuendelea kuboresha mazingira ya kidemokrasia, haki za binadamu na utawala wa sheria.